Polisi katika jimbo la Kwara katikati mwa Nigeria wanasema kuwa watu kumi wa familia moja wamekufa baada ya kunywa mchanganyiko wa mitishamba kama dawa ya jadi.
Ramani
Kisa hicho kilitokea katika kijiji cha Biogberu baada wanaume wawili kumfuata mwanamke mmoja aliyekuwa na ugonjwa wa miguu na kumpa mchanganyiko wa mitishamba kama tiba.
Lakini inasemekana walitoa sharti kwamba watu wote wa familia yake lazima watumie mchanganyiko huo ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa kati yao.
Katika taarifa siku ya Jumatano, msemaji wa polisi katika Jimbo lahe Kwara, Okasanmi Ajayi, wale wote waliokunywa dawa hiyo ya kienyeji baadaye walifariki.
Aliiambia BBC kwamba ‘mtu wa mwisho kati ya jamaa hao 10 wa familia moja amefariki’ akiwemo mgonjwa wa kwanza. Bw. Ajayi aliongeza kuwa muathiriwa mdogo alikuwa mtoto wa miaka miwili na mkubwa akiwa na miaka 40.
Polisi wanasema washukiwa wawili wamekamatwa na uchunguzi unaendelea. Haijabainika ikiwa ni wauguzi wa kienyeji kutoka jimii ya eneo hilo.
Baadhi ya Wanigeria hasa kutoka maeneo ya mashambani wanategemea tiba za kienyeji kutokana na ukosefu wa kujua kusoma na kuandika, imani ya kitamaduni na umasikini. Mfumo wa afya wa nchi hiyo pia unakabiliwa na changamoto kadhaa.
Post a Comment