Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wakuu wa wilaya nchini ambapo amewabadilisha vituo vya kazi baadhi yao na ameingiza sura mpya na kuwarudisha waliowahi kushika nafasi hizo na kuwaondoa wengine watatu katika nafasi zao.
Pichani kushoto ni Simon Odunga ambaye alikuwa mkuu wa Wilaya ya Rorya mkoani Mara kulia ni Richard Atufigwege Kasesela aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Iringa katikati ni Lengai Ole Sabaya ambaye alikuwa mkuu wa wilaya ya Hai.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Juni 19, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu, Rais Samia ameteua watu wa kada tofauti wengi wao wakiwa vijana.
Baadhi ya waliotoswa katika uteuzi huo ni pamoja na Lengai Ole Sabaya ambaye alikuwa mkuu wa wilaya ya Hai kabla ya kusimamishwa kwa tuhuma mbalimbali, Simon Odunga ambaye alikuwa mkuu wa Wilaya ya Rorya mkoani Mara pamoja na Richard Atufigwege Kasesela aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Iringa.
Vilevile, Rais Samia amewateua baadhi ya waliokuwa wabunge lakini kwa sababu mbalimbali wakashindwa kurejea bungeni. Wateule hao ni Joshua Nassari (Bunda), Halima Bulembo (Muheza) na Peter Lijualikali (Nkasi).
Post a Comment