Wahamiaji wakimbia Bangladesh kukwepa vizuizi vya Corona




Maelfu kwa maelfu ya wafanyakazi wahamiaji wameukimbia mji mkuu wa Bangladesh Dhaka leo Jumapili. 


Wafanyakazi hao wameondoka siku moja kabla kuanza kutekelezwa sheria kali za kudhibiti maambukizi ya Corona zitakazokwamisha shughuli za kiuchumi na kuwalazimisha watu kukaa majumbani huku maambukizi yakiongezeka. Shughuli za utoaji wa huduma za dharura na viwanda vinavyotengeza bidhaa zinazouzwa nje ya nchi zitaendelea kama kawaida. 



Wizara ya Afya ilisema maambukizi yalipungua mwezi Mei lakini yakaanza kuongezeka tena mwezi huu huku visa zaid ya 6000 vikiripotiwa siku ya Alhamisi na vifo 108 vikiripotiwa siku ya Ijumaa, Idadi hii inaelezwa kuwa kubwa katika kipindi cha zaidi ya miezi miwili. 



Wakati hayo yakiarifiwa Oman imeripoti rikodi ya maambukizi ya Covid-19 na vifo katika saa 72. Watu 119 wamekufa kutokana na ugonjwa huo huku jumla ya watu 5,517 wakigunduliwa kuambukizwa Corona katika kipindi hicho.




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post