Tundu Lissu Arejea




ALIYEKUWA Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA Tundu Lissu amewasili nchini Kenya akitokea Ubelgiji anapoishi kwa sasa, ambapo anatarajiwa kuzindua kitabu chake, Remaining in the Shadows: Parliament and Accountability in East Africa kesho jijini Nairobi.

 

Wakili wa Lissu, Profesa George Wajackoya akizungumza na Nation ameeleza kuwa Lissu ameshafika nchini Kenya na kwamba atahudhuria uzinduzi wa kitabu chake ” Remaining in the Shadows – Parliament and Accountability in East Africa “utakaofanyika katika hoteli ya Windsor 24.06.2021.

Makamu mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu amewasili jijini Nairobi, Kenya akitokea nchini Ubelgiji anakoishi ikielezwa kuwa yupo nchini humo kwa ajili ya uzinduzi wa kitabu chake cha Vivuli- Bunge na uwajibikaji kwa Afrika Mashariki.

 

Akizungumza na mtandao wa Nation Africa leo Alhamisi Juni 24, 2021 mwanasheria wake, Profesa George Wajackoya amethibitisha uwepo wa Lissu Nairobi na kwamba uzinduzi wa kitabu hicho utafanyika kesho Ijumaa.

 

“Ninatoa maelekezo aliyonipa kuthibitisha kwenu kuwa ni kweli yupo nchini kwa ajili ya kuzindua kitabu chake katika hoteli ya Windsor,” amesema Profesa Wacjakoya.

 

Lissu aliyegombea urais mwaka 2020 alinusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa risasi jijini Dodoma mwaka 2017 na hadi sasa watu waliomshambulia kwa risasi hawajatambuliwa huku akiwa amefanyiwa operesheni 25 hadi sasa.

 

Katika kitabu chake, anaeleza historia ya mabunge ya Tanzania, Kenya na Uganda. Akisimulia jinsi mabunge hayo yalivyotoka katika ukoloni wa Uingereza, anashauri mabunge hayo yawe na kivuli cha madaraka makubwa yaliyotolewa na watawala wa kikoloni na watawala waliokuja baada ya ukoloni.

“Ukiondoa Kenya kidogo, yaliyobaki yapo chini ya kivuli cha madaraka makubwa ya Rais,” anasema Lissu, kutokana na hali hiyo, anashauri uwepo wa demokrasia, uwajibikaji, utawala wa sheria na uhuru wa demokrasia kutawala.

 

Kitabu hicho kinakosoa mfumo wa utawala wa rais na kimetumia fasihi kikibeba ujumbe kutoka kwenye historia ya kisiasa na kikatiba ya nchi zote tatu.

 

“Kikileza kuondolewa kwa mfumo huo na madaraka yaliyomo, kitabu hicho kinatarajiwa kuibua mjadala ya kisiasa na kitaaluma. Ikiwa hivyo, kitakuwa kimetimiza lengo na kuhalalisha muda na gharama ya kukiandika,” inaeleza sehemu ya kitabu hicho.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post