Tunda Ajifungua Mtoto wa Kike





MUUZA nyago aliyejizolea umaarufu kutokana na vituko vyake katika mitandao ya kijamii, Tunda Sebastian amejifungua mtoto wa kike salama katika hospitali moja jijini Dar.

 

Tunda ambaye ni mpenzi wa msanii wa Bongo Fleva, Whozu kupitia insta story ya akaunti yake ya Instagram ametupia picha mbalimbali akiwa hospitalini na mama yake mzazi huku picha nyingine zikiambatana na pongeza kutoka kwa wadau mbalimbali kwa kujifungua Akizungumza na RISASI, mdau mkubwa wa sanaa aliyeomba hifadhi ya jina lake, alimuonya Tunda kupunguza starehe ili sasa amhudumie mtoto.



“Nimpongeze maana sasa nay eye amekuwa mama. Mama ni ulezi hivyo yale mambo ya ujana sasa apunguze. Apunguze starehe, apunguze mitoko ili aweze kumlea vizuri mwanaye,” alisema mdau huyo.Kwenye mitandao ya kijamii hususan Instagram, Tunda alipongezwa na mastaa mbalimbali pamoja wadau wengine.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post