Tessy Avunja Ukimya Bifu Na Aslay

 


SOSHOLAITI ambaye ni baby mama wa staa wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka, Kayitesy Abdul ‘Tessy’ amevunja ukimya juu ya kuwa na bifu na mzazi mwenzake huyo.

Tessy anasema, tofauti na watu wanavyomchukulia, lakini kwa upande wake yeye anamheshimu mno Aslay.

Tessy ambaye pia ni mwigizaji na mjasiriamali ameiambia IJUMAA SHOWBIZ kuwa, anashangaa kuona baadhi ya watu wanadai kuwa yeye na Aslay wana bifu, jambo ambalo siyo kweli na halitatokea.

“Kuna kitu ambacho watu hawakijui kutoka kwangu, mimi ni mtu mzima na ninajielewa hivyo kamwe siwezi kuwa na bifu na Aslay kwa sababu ni baba wa mtoto wangu.

Pia ninamsheshimu sana, isitoshe sisi tayari ni ndugu, kwa hiyo sidhani kama nikileta mambo yetu mitandaoni ndiyo nitapata suluhisho, zaidi ya kuonekana mjinga tu,” anasema Tessy ambaye amezaa motto mmoja wa kike na Aslay aitwaye Moza.

STORI: MEMORISE RICHARD



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post