Tasnia ya Habari Yakumbukwa Uteuzi wa Rais Wakuu wa Wilaya

  


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya zote nchini, ambapo katika teuzi hizo amegusa tasnia mbalimbali.

Pichani, Kulia ni Abdallah Mwaipaya wa ITV Mkuu wa Wilaya mteule wa Mwanga mkoani Kilimanjaro pamoja na Fatma Nyangasa ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya mteule wa Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Katika Tasnia ya Habari Rais amewateua Waandishi wa Habari mbalimbali. Miongoni mwa walioteuliwa ni Abdallah Mwaipaya wa ITV kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Pia yupo Fatma Nyangasa wa Azam TV kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es salaam, Gabriel Zakaria wa TBC kuwa Mkuu wa Wilaya ya Busega na Simon Simalenga wa Clouds kuwa Mkuu wa Wilaya ya Songwe.

Aidha wapo wanahabari ambao walikuwa tayari ni Wakuu wa Wilaya na wameteuliwa kuendelea ila wakibadilishiwa vituo vya kazi ambao ni Godwin Gondwe aliyehamishiwa Kinondoni kutoka Temeke na Jerry Muro aliyehamishiwa Ikungi Singida kutoka Arumeru.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post