Serikali imesitisha Mabadiliko ya Mitaala Mipya ya Masomo

 


Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga amesema kuwa serikali imesitisha kutumia mabadiliko ya mitaala mipya ya masomo katika shule za msingi na sekondari lengo likiwa ni kupokea maoni ya wadau wa elimu kuhusu maboresho ya mitaala kwa ngazi ya wawali, msingi na sekondari.

Amesema hayo wakati akifungua mkutano wa kupokea maoni ya wadau wa elimu Tanzania kuhusu uboreshwaji wa mitaala.

Mkutano huo wa siku moja umewakutanisha wadau wa elimu hapa nchi ili kutoa maoni ya mitaala ya elimu itakayo endana na sayansi.

Mkutano huo ambao utaibua hoja mbalimbali katika kuboresha mitaala ya elimu Tanzania, kutoka kwa wadau wa elimu kote nchini.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post