Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya Dkt. James Kihologwe, amesema kuwa takwimu zinaonesha kuwa watu 26 kati ya 100 wana matatizo ya shinikizo la juu la damu bila wao kujijua na kueleza kuwa inabaki tu hali ya kusikia mtu ameanguka.
Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya Dkt. James Kihologwe
Dkt. Kihogwe ameongeza kuwa takwimu za magonjwa yasiyo ya kuambukiza zinaonesha takribani watu 10 kati ya 100 wana tatizo la ugonjwa wa Kisukari ambapo asilimia 60 ya wagonjwa wa ugonjwa huo hawajui kama wanaumwa pia amesema watu 36 mpaka 22 wana mafuta mengi katika mishipa yao ya damu.
"Lakini zaidi ya robo tatu ya watu wenye shinikizo la juu la damu hawajijui kama wanatatizo hilo unasikia tu mtu amenguka hajijui," amesema Dkt. Kihologwe.
Dkt.Kihologwe amesema ameongeza kuwa yasiyoambukiza yamekuwa yakiongezeka nchini hivyo kupunguza maendeleo ya nchi ambapo amedai katika kila asilimia 10 ya ongezeko la magonjwa hayo yamekuwa yakipunguza pato la Taifa kwa asilimia 0.5.
Post a Comment