Msanii wa muziki wa bongo fleva Recho Kizunguzungu amesema kuwa habari zilizokuwa zinasambaa kwamba anatumia madawa ya kulevya zimesababisha kupoteza baadhi ya kazi alizokuwa akifanya kumuingizia pesa na kupelekea kuachwa na Boyfriend.
Amesema hayo wakati wa mahojiano katika kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio ambapo ameeleza kashfa hizo zilipelekea watu wake wa karibu kumacha na kubaki na mama yake tu.
“Sijui kwanini watu walikuwa wanazusha kwamba natumia madawa, zile story zilisababisha watu waliokuwa wananisaidia waache kunisaidia, kuna dili nilikuwa nimelipata ila baada ya story hizo likapotea mpaka Boyfriend akaniacha alibaki Mama tu” amesema Recho
“Hiyo ishu ya madawa ilianza baada ya mimi kuwa karibu na mtu anayetumia, nakumbuka tulikuwa kwenye show Dodoma na TID, akapiga picha ya kawaida tu na mimi nilikuwa pembeni, so story zikaanzia hapo” amesema Recho
Racho Kizunguzungu amerudi tena kwenye game ya muziki baada ya ukimya wa muda mrefu ambapo ameachia wimbo unaoenda kwa jina lwa nikune.
Post a Comment