Ray Kigosi "Sibadilishi wa Kuzaa Naye, Mtoto wa Pili Nitarudi Pale Pale"





MWIGIZAJI mkubwa kunako Bongo Movies, Vincent Kigosi almaarufu Ray anasema kuwa, hana mpango wa kubadilisha mwanamke wa kuzaa naye watoto wake wengine.


Ikumbukwe kwamba, Ray amezaa mtoto mmoja wa kiume na staa mwenzake wa Bongo Movies, Chuchu Hans aitwaye Jayden.

Akistorisha na Gazeti la IJUMAA katika mahojiano maalum, Ray anasema kuwa, anajivunia mno na kumshukuru Mungu kwa kupata mtoto wa kiume wa kwanza kutoka kwa Chuchu hivyo hategemei kwenda kuzaa na mwanamke mwingine.


“Sidhani kama naweza kuzaa mtoto mwingine kwa mwanamke mwingine, hilo siwezi na hata halipo kwenye kichwa changu. Nilipozaa wa kwanza ndipo nitakapozaa tena hapohapo,” anasema Ray.


Ray na Chuchu walianzisha uhusiano wa siri tangu kitambo, lakini baadaye waliweka wazi baada kubarikiwa kupata mtoto wao huyo wa kiume.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post