Rais wa kwanza wa Zambia afariki




Mmoja ya watu maarufu zaidi barani Afrika na mpiganiaji uhuru,Rais wa zamani wa Zambia Kenneth Kaunda ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 97.



Kaunda alikimbizwa katika hospitali moja mjini Lusaka mapema wiki hii na kulazwa baada ya kuugua homa ya mapafu.

Mwaka 1950 , bwana Kaunda alikuwa mtu muhimu katika Vuguvu la kupigania uhuru wa Rhodesia ya kaskazini kutoka kwa Uingereza.

Alikuwa Rais wa kwanza wa Zambia mwaka 1964 na kuongoza taifa hilo kupitia miongo kadhaa ya utawala wa chama kimoja.

Bwana Kaunda alikuwa shabiki mkubwa wa juhudi za kumaliza ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini na alikuwa pia akiongoza mavuguvugu nchini Msumbiji na nchini Zimbabwe.

By –BAKARI WAZIRI


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post