R. Kelly Ahamishwa Gereza

 


Mwimbaji wa muziki wa RnB, R. Kelly amehamishiwa Gereza lililopo mjini Brooklyn, New York ambapo atakuwa hapo kabla ya kesi kuanza kusikilizwa mwezi Agosti mwaka huu.

Tovuti ya Magereza imethibitisha kuwa siku ya Jumatano wiki hii Kelly alikuwa tayari amewasili katika Gereza la Metropolitan Detention Center huko Brooklyn.

Tangu mwaka 2019 R. Kelly alikuwa akishikiliwa katika Gereza la MCC kwa makosa matatu ikiwemo la unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wenye umri mdogo.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post