SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Job Ndugai amewaonya wanaotoa taarifa za upotoshaji zenye lengo la kulichafua Bunge kuacha kufanya hivyo kwa kuwa sasa hatua zitaanza kuchukuliwa ikiwemo kuitwa kwenye kamati ya maadili ya Bunge.
Spika Ndugai ameyasema hayo bungeni Dodoma leo, Juni 25,2021 wakati akitolea ufafanuzi wa orodha inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha majina ya waliokuwa wabunge wa Bunge la 11 likiwemo la Tundu Lissu kuwa wanalidai Bunge hivyo walipwe.
Ndugai amesema taarifa hiyo ni ya uongo kwa kuwa ilikuwa ya mwaka 2018 na kwamba hakuna mbunge wala aliyekuwa mbunge hata mmoja anayelidai Bunge.
Post a Comment