Jeshi la Polisi nchini #Uganda, linachunguza mauaji ya Ester Naula (13) ambaye amedaiwa kupigwa risasi na Polisi kwa kukutwa nje saa moja na robo usiku ambao ni muda wa kuwa ndani
Tukio hilo limetokea katika Wilaya ya Butaleja, ambapo inaelezwa kuwa Ester alikuwa ametoka kununua chapati ndipo Polisi alirusha risasi baada ya Ester na Wananchi wengine kukimbia ili kuepuka kukamtwa
Aidha, Msemaji wa Polisi wa Mkoa wa Kusini, Moses Mugwe amethibitisha tukio hilo lililoacha majeruhi kadhaa. Polisi aliyefanya tukio hilo ameshakamatwa
Post a Comment