Mtoto anyongwa Mpaka KUFA na Mfanyakazi wa Ndani Huko Arusha


Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia msichana mmoja, (jina linahifadhiwa) mwenyeji wa mkoa wa Mara kwa tuhuma za kumuua mtoto ambaye ametambulika kwa Jina la Tifan Osward mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.

Taarifa za awali zinaonyesha binti huyo  ni msaidizi wa kazi za ndani, na  ameajiriwa takriban miezi miwili iliyopita.

Tukio hilo limetokea Juni 19,2021 mnamo majira ya saa kumi na mbili za jioni ,ambapo binti huyo alikua ameachwa na mtoto nyumbani.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linaendela na uchunguzi kujua chanzo na sababu za tukio hilo na mara tu uchunguzi utakapokamilika watalifikisha mbele ya vyombo vya sheria.

Aidha Jeshi la polisi Mkoa wa Arusha ,linatoa wito kwa wazazi na walezi kufuatilia mienendo ya wasaidizi wao wa kazi za ndani, kabla na baada ya kuwachukua ili iwasaidie kufahamu kwa kina ili pindi wanapowachukua wasaidizi hao yasitokee madhara kwa watoto na familia zao pindi wanapowaacha nyumbani.








0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post