Mobetto Afunguka Mondi Kwenda Kwake "Siwezi Mkaribisha Mwanaume Kwangu"




Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya nchini na mfanyabiashara Hamisa Hassan ‘Mobetto’ ambaye pia ni mzazi mwenza wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul ‘Dimaond platinum’amesema kuwa Diamond hawezi kwenda kwake hata siku moja.

Hili limezuka baada ya Mwanamama mjasiriamali kutoka nchini Uganda,Zarinah Hassan’Zari The Bossylady’ kila wakati akionekana kutembelewa na Mondi kwa ajili ya kusalimia baba.

MASHABIKI WAMBIPU MOBETTO

Kama tunavyofahamu watu wa kwenye mitandao hawakosi kuwa na chokochoka, wameanza kumchokonoa mwanamama huyu kwa vijimaneno ya chinichini kuwa na yeye lini Mondi ataenda kwake kwa ajili ya kumsalimia Dyllan?

“lini shoga yetu nae atafatwa na chibu kwake kwa ajili ya kwenda kumsalimia mwane Dyllan kama anavyofanya kwenda kwa Zari maana wapenzi watazamaji tunaona tu kaka kakazani kwelikweli kwenda South.


“Au ndiyo kusema kwamba anajimudu haitaji msaada wa jezi kiwanda anacho ndani ila kama ni mimi ningeumia sana roh’.alisema mpashaji huyo.

MOBETTO AWATOLEA UVIVU

Baada ya mambo kuwa mengi kwenye mitandao ya kijamii ya kumtaka mwanamama huyo amkaribishe Diamond kwake kwa ajili ya kumsalimia na kucheza na mwanae.

Mobetto alijibu kwa kujiamini kwamba nyumbani kwake hawezi kumleta mwanaume kwanza anaishi na mama yae.


“ Nyumbani kwangu hapana kabisa mwanume kuja kwanza mwanaume ambaye sina uhusianao nae wa kimapenzi,kwanza mimi najihudumia kila kitu mwenyewe ila mwanae anamuhudumia sasa atakuja kwa ajili ya nini haswa na pia kwenye nyumba yangu mimi naishi na mama yangu mzazi kwahiyo mtu hadi aje nyumbani kwangu anatakiwa awe na sababu ya msingi mno, siwezi pia kuongelea ule upande mwingine (South Afrika) kwa sababu siamini kama pananihusu,” alisema Mobetto.

Stori: Khadija Bakari


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post