Mmiliki wa gari ajali ya Morogoro ajisalimisha polisi




Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro,  Fortunatus Muslimu amesema mmiliki wa gari lililosababisha vifo vya watu tisa  iliyotokea eneo la Oil com, Nanenane  Manispaa ya Morogoro amejisalimisha polisi.



Taarifa hiyo imetolewa  leo Jumanne, Juni 29, 2021 katika mkutano wake na waandishi wa habari kwenye  kituo kikuu cha Mabasi Msamvu  wakati wa Operesheni maalumu ya ukaguzi wa  Mabasi ya abiria.

Kamanda Muslimu amesema katika  operesheni hiyo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo,wamekamata magari 36 ambayo hayakuwa na vibali vya kusafiri.

Aidha,amebainisha kuwa magari mengi yamekuwa yakiwekwa mashada ya maua na picha zinazoonyesha  kuwa ni za marehemu huku wahusika wakieleza kuwa wanasafirisha msiba wakati wanajua kuwa si kweli


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post