Mke wa aliyekuwa Mchezaji maarufu wa Mpira wa kikapu Kobe Bryant, Vanessa Bryant ameripotiwa kumaliza shauri lake dhidi ya rubani na wamiliki wa helikopta ambayo ilichukua uhai wa mume wake pamoja na binti yake kwenye ajali iliyotokea Januari 26, 2020 mjini Los Angeles na kuua watu wengine 7.
Juzi Jumanne Vanessa Bryant pamoja na ndugu wengine wa marehemu waliamua kulimaliza shauri hilo kwa kukubaliana pande zote mbili kutofika mahakamani.
Hata hivyo vipengele vya maridhiano yao havijawekwa wazi kama ni fidia kiasi gani watalipwa. Kama makubaliano hayo yatapitishwa na Mahakama, itakuwa ndio mwisho wa kesi hiyo juu ya kampuni ya helikopta pamoja na rubani wake.
Post a Comment