Katika kipindi cha miaka miwili tu Johnny Boufarhat amegeuza jukwaa lake la mtandao la kupokea mikutano linalofahamika kama Hopin, kuwa kampuni yenye thamani ya zaidi ya pauni bilioni nne.
Anawaajiri watu 500, lakini baadhi yao hajawahi hata kukutana nao, kutoka ofisi kuu.
Kulingana na orodha ya jarida la The Sunday Times la watu tajiri linalochapishwa nchini Uingereza, kijana huyu mwenye umri wa miaka 27 tu kwa sasa ndiye tajiri kijana zaidi aliyejiwezesha mwenyewe kuwa bilionea .
Aidha mchango aliouchangisha hivi karibuni kupitia kampuni yake Hopin ulifikia pauni milioni 400 kutoka kwa wawekezaji binafsi, na hivyo kumfanya kuwa na utajiri wenye thamani ya dolabilioni $5.65 (£4.05bn).
Lakini hupenda kufanya mambo tofauti
“Kuwa kampuni inayofanya kazi yote kwa njia ya mtandao inatusaidia kufanya mambo mengine ambayo kampuni nyingine hazijaweza kuyafanya kabla ,” anaeleza Johnny Boufarhat, kutoka katika nyumba zake alizonunua hivi karibuni za kupangisha zilizpo katika jiji la Barcelona, Uhispania.
Licha ya kutokuwa na ofisi ya kudumu, mjasiliamali huyu wala hana nyumba au makazi ya kudumu .
Ni mtumiaji wa Digital/ mtandao wa kuhama hama kutoka moja wapo ya nyumba zake za kupangisha kwenye eneo moja na kuhamia kwenye nyumba moja nyingine kati ya nyumba zake za kupangisha, akiendesha kampuni yake kutoka pale alipo kwa wakati huo.
Post a Comment