Metacha Aomba Msamaha Yanga





KIPA  wa Klabu ya Yanga, Metacha Mnata ameomba radhi kwa kitendo kisicho cha kiungwana alichokionesha kwa mashabiki wa klabu yake  jana Juni 17, baada ya kuzomewa kwenye mchezo wa Ligi Kuu ambao wanajangwani walishinda bao 3-2 dhidi ya Ruvu Shooting.

 

”Kwa niaba ya Familia yangu, Management yangu na mimi mwenyewe napenda kuchukua fursa hii kuomba msamaha kwa Viongozi wa Klabu yangu ya Yanga SC, Wachezaji wenzangu, Benchi la Ufundi, Mashabiki wa Klabu ya Yanga, Mamlaka za soka nchini na wadau wote soka ambao wamekwazika kwa kwa kitendo nilichokifanya jana.”

 

”Nikiri hakikuwa kitendo cha kiungwana hivyo najutia makosa niliyoyafanya. Mimi kama mchezaji wa Yanga na Timu ya Taifa napaswa kuwa mfano mzuri siku zote mbele za watoto na wanaotamani kuwa kama mimi na watu ambao aidha walikuwepo kiwanjani au waliona mechi kupitia Televisheni majumbani kwao”.

 

”Natambua mchango na umuhimu wa mashabiki kwangu binafsi na kwa Klabu, hivyo kitendo kile hakikupaswa kutokea.”ameandika Metacha Mnata kupitia Ukurasa wake kwenye  wa Instagram


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post