MCT yalaani Waandishi wa habari kutishiwa





Baraza la Habari Tanzania (MCT) linalaani vikali kitendo cha watu wasiojulikana kuwatisha waandishi wa habari wa ITV, TBC na Mwananchi kutokana na kuandika habari zinazomhusu aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, anayetuhumiwa kwa makosa mbali mbali mahakamani.
Akizungumza leo, Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga, amesema Baraza limepokea taarifa hizo kwa mshtuko mkubwa hasa ikizingatiwa kuwa Mei 20, 2021 katika Mkutano Mkuu wa Wahariri mjini Morogoro, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alisema Serikali haitakubali kuona waandishi wa habari wakinyanyaswa.

Alisema Katika hotuba yake hiyo, Waziri Mkuu aliongeza kusema kuwa “Siyo sera ya Serikali kunyanyasa waandishi wa habari” alinukuu Kajubi.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post