Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Aikael Mbowe anashangazwa na kitendo cha Rais wa Jmamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan kutokutana na vyama vya Siasa vya Upinzani mpaka hivi leo ,ikiwa ni zaidi ya miezi mitatu tangu kuapishwa kwake.
Mbowe ameyasema hayo katika mahojiano aliyofanya na Shirika la Habari la Uingeeza (BBC),leo june 25,2021.
“Mojawapo ya kauli za awali kabisa baada ya Mama kupata Mamlaka ya kuongoza taifa letu,ni lengo lake la kukutana na sisi,na mimi binafsi kama mwenyekiti wa CHADEMA,nilimuandikia barua na Katibu wa Rais alinijibu kwamba Mama amepokea barua yenu na ameridhia kukutana na CHADEMA,kwa hiyo tuliamini ni vyema Mama anapoingia kwenye nafasi atoe kipaumbele kwa Chama kikuu cha upinzani ambacho ni muhanga mkubwa wa Siasa za nchi hii”amesema Mbowe.
Mbowe aliendela kusema kuwa Rais amekutana na makundi mbali mbali,kitu ambacho si jambo baya lakini walitarajia angeanza kukutana na vyama vya upinzani kwanza, ili pindi anapoendelea na majukumu yake atende kwa kufuata mapendekezo ,hoja ama ushauri kutoka kwetu.
Mapema mwaka huu baada ya Rais Samia kupewa mamlaka ,katika hotuba zake za mwanzo aliahidi kukutna na viongozi wa Vyama vya Siasa nchini lakini Viongozi hao wanashangazwa na jambo hilo kutofanyika mpaka leo.
Post a Comment