Kutoka Kwa Mdau:
Nimeangalia Interview vizuri mwanzo mpaka mwisho na nimekuja na maoni yangu, ikumbukwe maoni yangu sio sheria naongea nilichokiona.
Kwanza niwapongeze sana Mama Dangote, Esma Platnumz pamoja na @diamondplatnumz Simba Baba Lao, jamani kwa mtu kama Diamond watu wanaoomba msaada kwake ni wengi, tukio la kumchukua mtoto tu na kuamua kuishi nae tu ni ubinadamu. Kwa maana huku mtaani wapo watoto wangapi wanalala nje?? Sisi watanzania wa kawaida tumewahi kuguswa hata kumchukua mmoja tukaishi nae?? Tuachie Mbali kumsomesha ambako mtoto ndio dream yake, swala la kusomesha ni Kipengele sana, then mtoto katoka Kongo kuja Bongo haeleweki amekujaje hana wazazi?? Kwanini mtoto wa miaka 14 akimbilie Tz, Congo wapo mastaa na matajiri kibao kama ni swala la kusoma nadhani Congo was much Best kuliko Tanzania.
Napata ukakasi inasema mtoto sio kawaida yake kutembea kwa miguu ila alichukua Ipad that day akaamua aende kwa Diamond kumsalimia kwanini hakuaga?? Na kwanini aliondoka na kitu cha mtu mwingine hata kama walikuwa wanatumia wote ila kidogo hapo kuna shida. Sijajua mfumo wa usomaji hapa Bongo upoje ila ili asome si inabidi wapete ufaulu wake au inakuwaje?? 😂😂Niache nako sina taalum sana huko.
Kwamba Mama Dangote aliamuru mtoto auawe kwasababu ya Ipad nakata 😂😂😂, ila kusema aachwe huko nakubali maana Connection yake na Familia haikuwa kubwa so nadhani Wakaona huyu anatuletea matatizo wakatua mzigo. Kumradhi ndugu waandishi nadhani kuna kitu kidogo mumeongeza hapo mwishoni la kumwajili, ikumbukwe mtoto alisaidiwa sio kwamba alienda kufanya kazi, na Mama Dangote hakumchukua kama Mfanyakazi ila alimchukua ila amsaidie kumuhifadhi.
12 mtoto anasema ameishi nao vizuri kipindi chote ila isipokuwa baada ya Ipad ndipo tatzo lilianzia hapo. Sasa swala la kusema kumfanyisha mtoto chini ya Umri wa miaka 14 sio sawa alikuwa anaishi kama mtoto hivyo kwa watoto wa miaka 14 kwenu hawadeki?? Hawaoshi vyombo?? Sema Sasa hao Security ndio wamezingua, sitaki kujua kama waliagizwa au la sio kila agizo unatii kuna vitu unaweza kuchekecha.
Post a Comment