Mange Kimambi "Gari ya Escalade Manigga Wote in the Hood Wanazo Mpaka sisi Wandengereko Tuliozamia Marekani Tunazo"


Reposted from @mangekimambi_ Leo elimu ntawapa tu mtake msitake. 🤣🤣🤣

Kuna mtu kanitumia hii anasema mbona na Drake anayo Escalade kama sio gari ya matajiri? jamani inabidi muelewe culture ya wamarekani na hii gari ya Escalade. Hii gari inapendwa na wanaume especially ma-black Americans. Huko kwenye hood hizi gari ndo huzikosi, hizi gari marekani ni cultural status na sio status ya utajiri. It’s considered a cool car not an expensive car. Na hii gari inatengenezwa marekani so wenyewe mastaaa wanasapoti kitu chao, wanajivunia. Ni kama hapo bongo Mo Dewji avae kitenge ambacho hata houseboy wako huwa anashonaga. Ila still Mo Dewji ataonekana cool sababu kitenge kinaonekana ni cultural status sio status ya pesa, na watu wanavaa vitenge sababu wanavipenda sio sababu hawana hela ya kuvaa nguo expensive. Ndo mastaaa wa marekani na hii gari ya Escalade, hii gari wanaendesha sababu wanaipenda sio sababu ni gari ya kuwaonyesha wao ni matajiri. Hii gari kwa marekani ni sawa na vitenge Tanzania, wanavaa matajiri kwa maskini na havitoki kwenye fashion .

Hii gari kina Drake wanaiendesha siku wakiwa wanataka tu kuonekana cool na pia wafans wanafurahi kuona star wao anaendesha gari kama kama lake au ambalo hata baba yake analo. Wanaonekana na mafans wako humble hawajisikiiii.

Drake hatembei na Escalade kuonyesha kuwa yeye ni Drake ana pesa ndefu. Drake anatembea na Escalade ku connect na fans wake na kuendesha gari ambayo roho yake inapenda.

Siku Drake akitaka kutuonyesha kuwa yeye ni Drake ana pesa mtiririko huwa anatutokea na gari hizo hapo nilizowawekea. Fanyeni kuswipe. Hizi ndo gari zake za kuwaonyesha wana muziki wengine marekani hawampatiii kwa utajiri🤣🤣🤣. Hizo ndo gari zake za show off. Sio Escalade ambazo manigga wote in the hood wanazo. Mpaka sisi wandengereko tuliozamia marekani tunazo.

Na Drake huwa haposti gari zake expensive, hataki kuwaringishia mafans, huwa anaposti gari kama hizi ambazo na sisi kajamba nani tuna afford. Hizo expensive huwa tunafanya kuonyeshwa namablog a.k.a wambea wa marekani.

Dai alitakiwa kuwa na hii gari just for fun just because he can, na sio kwamba ndo gari yake ya kindaki ndaki ya kusifiwa ana pesa. Hapana jamani.

Hiyo ndo tofauti iliyopo.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post