Mambo 10 nilioyaona Azam FC vs Simba



1: MECHI DUME. Mechi ya Jasho na Damu. Mechi ya kibabe iliyoamuliwa kikubwa💪 Uzoefu/ kasi ya kufikiri kwa Morisson imewapa Azam kilio kisichokuwa na pole


2: Ni CLEAR GOAL.. Quick Restart ni haki ya waliotendewa madhambi, sio waliocheza madhambi. Waliochezewa rafu ndio wanaotakiwa kuomba 'Ukuta' sio waliocheza. Refa angeweza kukataa lile bao kama kungekuwa na makosa kwenye kuanzisha.. WELL DONE refa ARAJIGA 👏


3: Naweza kusema kila kitu kuhusu mbinu za Lwandamina lakini credit kubwa ni kwa wachezaji wa Azam FC. Walicheza kwa ajili ya Klabu. Walikubali kuwa watumwa kiwanjani. Walikimbia kilomita nyingi sana kupunguza madhara ya Simba. Huwa ni nadra sana kuwaona Azam kwenye morali ile. Hii ni ishara waliandaliwa vyema kisaiokolojia.


4: Didier Gomes👏 Again, ameonyesha uhodari wake wa kuswitch Tactics zake kiwanjani. 'Sub' dume ni ya kumtoa Bwalya na kumuingiza Morrison. Si kwa sababu ya Asist ya Morisson.. Ni kwa sababu ya namna alivyochange role ya Chama kiwanjani. Kivipi?


5: Chama ni master kwenye zone ya 14🙌 Kucheza mbele ya uso wa goli kuliwafanya viungo wawili wa chini wa Azam kusogea zaidi na line yao. Hii ikatengeneza 1v1 kwenye eneo la mwisho la Azam. Kwa Quality ya Simba, ukiwaacha kwenye 1v1, Lazima wakuhukumu


6: Aggrey Morris🙌 Kiwango bora kiwanjani. Busara kubwa kichwani. Alimpa Bocco mechi ngumu sana. Sauti yake ilikuwa alart kwa kuwafanya wenzake kuwa makini


7: Onyango🙌 Mtu chuma kweli kweli. Alipokea kila changamoto aliyopewa na Chirwa. Aliimeza presha ya Azam na kudili nayo kibabe


8: Mudathit Yahya,, Bryson.. WOW🙌 Jasho walilomwaga linatosha kutumika kama kipimo cha wachezaji wapya watakaokuja Azam.. Umia kwa ajili ya Timu yako. What A Perfomance


9: Morrison🙌 Mbali na Asisti aliyotoa, kasi yake ilikuja kumpa mtihani mgumu sana Bruce Kangwa. Miguu yake ilikimbia sawa na ubongo wake.


10: Well Done refa Arajiga. Mechi ilikuwa na presha kubwa. Ikatawaliwa na ubabe lakini aliumudu mchezo kikubwa sana.


Nb: Mwana Kuyataka ...



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post