Mama mzazi wa kiungo wa Simba, Jonas Mkude Asikitishwa na Mwanawe Kutakiwa Kwenda Kupima Akili


Mama mzazi wa kiungo wa Simba, Jonas Mkude, Grace Shimba amezungumzia msala alionao mwanae hasa ishu ya kutakiwa kwenda kupimwa.

“Imeniumiza sana kwani nimemzaa Jonas akiwa na akili timamu na nimeyaona yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii yananipa mawazo ila sina chakufanya”

“Utumbo unanikata kwani nimembeba miezi tisa tumboni kwangu, ilinishtua sana kuambiwa anatakiwa kwenda kupima wengine wakidai akili, ila namuombea kwa Mungu amlinde.”

“Nilimzaa akiwa mzima, pia anapaswa kumuomba Mungu amsimamie, ujue siwezi kuingilia mambo ya ajira yake ila imenigusa kuhusu akili yake,”

“Asubiri maamuzi na klabu, ndio maana nimesema hilo siwezi kuliingilia, pia anapaswa kunyamaza kimya na sio kujibizana na kila mtu,”

Mkude alinza kucheza kikosi cha kwanza cha Simba msimu wa 2011


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post