Ndoa ya pili ya Penina Kyalo ilikuwa kwenye mume wa ndoto zake
Mambo yaligeuka baada yake kujifungua mwanao wa kwanza
Ni miaka 23 tangu alipolishwa mahaba na mumewe ambaye baadaye alimruhusu kuchovya asali nje
Baada ya kusambaratika kwa ndoa yake ya kwanza, Penina Mueni Kyalo alikutana na mume wa pili ambaye kulinga naye alikuwa jamaa wa ndoto zake.
Mume Wangu Hajaniguza kwa Miaka 23, Alinipa Ruhusa ya Kurina Asali Nje
Licha ya kukosa penzi kwa miaka 23, Penina Kyalo anajivunia kuheshimu mwili wake.
Alikuwa mwanajeshi, hakuwa akinywa pombe, alikuwa mcha Mungu na alimpa penzi la dhati kama alivyotaka.
Haikuchukua muda mrefu kabla ya wawili hao kuanza kuishi pamoja na mnamo 1993 alipata ujauzito wa kifungua mimba wao.
"Alikuwa mtu mzuri sana. Baada yangu kushika ujauzito, alikuwa akinisaidia kufua. Alikuwa na mtu mwenye roho safi sana," alimwambia Lynn Ngugi.
Hata hivyo siku zake za raha hazikudumu kwa muda mrefu kwani kutokana na ujauzito alianza kuchoka kwenda nje kujivinjari kama alivyozoea na mumewe.
Hapo ndipo mumewe alipoanza kuingia kwenye mahusiano na mmoja wa marafiki zake wa miaka mingi, na ambaye alimwona kama dada.
"Mtu alikuja na kuniarifu napaswa kuwa macho kwani rafiki yangu wa karibu alikuwa akimyemelea mume wangu," alisimulia.
Mambo yalizidi kuwa mabaya baada ya kujifungua wakati Peninah aligundua kuwa mumewe huenda aliingia nymbani kwake na kuondoka kisiri wakati alikuwa hayupo na mara kwa mara alikuwa akiepuka kuwa na uhusiano wa kimapenzi naye.
Alipochoka kusubiri kwa muda mrefu na kumkabili, naye akamuarifu kwmaba licha ya kuwa yeye ni mrembo na mama wa mwanao haja ya kushiriki mapenzi naye ilikuwa imemuondoka.
"Nyakati zile chache ambazo tulijaribu kushiriki penzi alikuwa akiniita jina la mwanamke mwingine hususan Nyambura," aliongeza.
Mama huyo alijikuta katika hali ngumu kwani hakuwa na rafiki hata mmoja wa kuaminika ambaye angemfichulia aliyokuwa akiyapitia kwani huenda wangetumia fursa hiyo kumvizia mumewe.
Penina hatimaye alijua kwamba ndoa yake imefika kikomo wakati baba wa mwanawe alimruhusu kushiriki mahaba nje ya ndoa yao.
"Aliniambia niwe na uhusiano wa kimapenzi na mtu yeyote ninayetaka na hatawahi kunizuia," alisema.
Anawashauri watu ambao wako kwenye ndoa zilizo na matatizo wapaze sauti wasikike ili nao wapate msaada.
Alisema kwamba amejizuia kuzurura nje ya ndoa kutokana na nidhamu yake na kwa sababu anamcha Mungu lakini anajutia muda aliopoteza.
"Ningependa kupata zaidi ya mtoto mmoja, lakini sasa nina zaidi ya miaka 50, tayari muda umesonga sana na siwezi kujiiingiza katika maamuzi kama hayo," alifunua.
Jambo moja ambalo linamfanya Peninah ajivunie ni kwamba amejiheshimu kwa miongo miwili licha ya kuruhusiwa kutafuta mahaba kwingine.
Post a Comment