Mwanza. Hospitali ya rufaa ya Kanda ya Bugando imepoteza madaktari bingwa wawili katika kipindi cha wiki moja.
Madaktari hao ni Ronald Hodge raia wa Cuba bingwa wa mishipa ya fahamu na ubongo aliyefariki dunia Juni 17, 2021 na Daniel Gunda, bingwa wa magonjwa ya ndani ambaye pia ni mkufunzi mwandamizi wa chuo kikuu cha Katoliki cha afya na sayansi shirikishi aliyefariki dunia Juni 24, 2021.
Akizungumza na Mwananchi Digital leo Ijumaa Juni 25, 2021 kaimu mkurugenzi mkuu wa hospitali hiyo, Dk Fabian Massaga amethibitisha vifo hivyo.
“Ni kweli tumepoteza madaktari bingwa wawili ila taarifa za chanzo cha vifo cha binadamu yoyote huwa kuna utaratibu wa kufuata kwa hiyo ni vyema ukafika ofisini kwangu wiki ijayo maana sasa hivi mimi siko ofisini niko safarini Dodoma,” amesema Dk Massaga.
Post a Comment