Jamaa mmoja amewaacha wengi mdomo wazi baada ya kuonekana kwenye pikipiki ya afisa wa polisi wa trafiki wakati afisa huyo wa trafiki alipoacha pikipiki yake na kuanza kuondoa msongamano wa magari kwenye barabara.
Maafisa wa polisi Kenya huwa wanaheshimika pakubwa na vifaa vyao vya kazi hutazamiwa kwa umbali na raia.
Hata hivyo, jamaa mmoja jijini aliamua liwe liwalo na akachukua pikipiki iliyokuwa imeegeshwa na afisa huyo huku akitembea kwa mguu ili kusaidia kuondoa msongamano wa magari.
Abiria waliokuwa kwenye magari walibaki kinywa wazi huku wengine wakichomoa simu zao na kunasa kisa hicho.
Kwenye picha zilizopakiwa katika mtandao, Raia huyo alionekana akiwa kwenye pikipiki huku baadhi ya wahudumu wakibaki kushangaa kilichokuwa kikiendelea.
"Leo jamaa ameamua kuingia kituo cha polisi na kuchukua usukani. Kweli hii Nairobi watu wanakula dawa," aliandika John Maina ambaye ni mhudumu wa matatu.
Baada ya muda afisa huyo anagundua kuwa pikipiki yake iko chini ya mikono ya raia na anakimbia kumkabili jamaa huyo.
Anaonekana akimfurusha kutoka mali hiyo ya serikali kwa ukali huku wapita njia nao wakifurahia nipe nikupe zao.
Kulingana na walioshuhudia kisa hicho, jamaa huyo alionekana mwenye matatizo ya kiakili kwa kiasi fulani.
"Ni jamaa amekula dawa kweli kweli, alishindwa ni vipi atatembea ilhali afisa ameacha pikipiki hiyo," Felix Odipo alisema
Post a Comment