Irene Uwoya Ageuka Pedeshee wa Kike Bongo, Wadau Wahoji Chanzo Chake cha Pesa




SIKU za hivi karibuni Irene Uwoya amekuwa pedeshee wa kike, anamwaga mawe ile mbaya.
Wakati wa Komunio ya mwanaye, Irene alimtunza mama yake mzazi minoti hadi ardhi ikageuka wekundu wa msimbazi na Jana kwenye harusi ya Dida pale Mlimani City alikichafua kwa fedha.
Nyuma ya matukio yake ya kula bata mwigizaji huyo amekuwa akijitokeza mara kadhaa akilalamika kuonewa “kijicho”.


Kwa mfano, kwenye ukurasa wake wa Instagram leo ameandika maneno haya hata kama hakumaanisha ni yeye lakini kwa tafsiri anajizungumzia:


Wakijaribu kukushusha… kukutukana … kukuharibia heshima yako …nyamaza na usiongee unayoyajua kuhusu wao sababu hicho ndio kinakufanya kuwa tofauti na utofauti wako ndio nguvu yako.


Kwa nini Uwoya anasakamwa? Anasakamwa kwa sababu mafanikio yanayoonekana kwake yamekuwa ndiyo mchawi wake.


Mafanikio mara zote yana kelele nyingi na hasa yakiambatana na “kujionesha.”
Kikubwa watu wanajiuliza: “Irene Uwoya huyu tunayemfahamu fedha za kumwagamwaga anazipata wapi?”
Hapo sasa ndipo linapokuja suala la “anajiuza” “Kapata tajiri mwenye kiwanda kikubwa Bongo” “Anauza unga” “Kamshika kigogo wa serikali” na maneno kama hayo.


Lakini kubwa kama siyo mzizi wa yote ni kwamba kazi anayofanya Irene Uwoya haionekani, ni kama mtu anavuna asichopanda.


Sijui wewe ungemshauri nini Irene Uwoya hasa pale anapolialia kusakamwa na kuharibiwa heshima yake kwenye jamii? Na pengine unajua mihela anaipata wapi na kwa kazi gazi?


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post