Idadi ya vifo ajali iliyotokea usiku wa Juni 21 baada ya magari matatu kugongana ikiwemo Toyota Coaster, Toyota Cresta na lori imeongezeka na kufikia 9 ambapo awali ilikuwa watano huku majeruhi wakiwa 23.
Akithibitisha kuongezeka kwa idadi ya vifo, Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, Dr. Kesy Ngalawa amesema kati ya hao majeruhi watano wapo chumba maalum cha uangalizi (ICU).
Kwa upande wake mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo Frank Ramsoni amesema gari hiyo ya Coaster ilikua inatoka DSM kuelekea Mbeya walipofika njiani dereva aliweka mashada kwenye gari hilo kama ishara imebeba maiti ili kupata wepesi wa kufanya safari ambapo baada ya kufika eneo la Kingulwira Manispaa ya Morogoro gari hiyo ilisimamishwa na Askari.
Baada ya kusimamishwa na Askari dereva wa gari hilo alishuka kisha Msaidizi wake alichukua gari na kuondoa bila ruhusa ya Askari.
Walipofika eneo la Oil Com dereva wa gari alimpigia simu mwenzake ambaye alibaki na Askari alimpigia wakati huo gari ikiwa kwenye mwendokasi baada ya kupokea simu ndipo gari ikapoteza mwelekeo na kugongana uso kwa uso na lori ambalo ni Kampuni ya Dangote.
Post a Comment