Hesabu za Simba Kuwa Mabingwa wa Ligi Kuu Hizi Hapa, Yanga Walie tu

 


Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara, wekundu wa msimbazi Simba, wanakaribia kuutwaa ubingwa wa VPL kwa msimu wa nne mfululizo baada ya jioni ya leo kuitandika Polisi Tanzania bao 1-0.

Bao pekee la Simba lilifungwa na Luis Miquissone aliyecheka na nyavu dakika ya 28 ya mchezo bao lililodumu kwa dakika zote tisini za mchezo huo pekee wa leo.

Ushindi huo umewafanya Simba ambao ndio vinara, kufikisha alama 70 baada ya kucheza michezo 28, na wanahitaji alama 7 pekee ambazo hazitofikiwa na timu yoyote ile katika Ligi Kuu.

Yanga ndiyo timu iliyo katika nafasi ya pili wakiwa na alama 64 na iwapo watashinda michezo yote minne iliyosalia, wataishia kuwa na alama 76 



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post