Herbinder Seth Atakiwa Kutokutoka Nchini Kwa Kipindi Cha Mwaka Mmoja





Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kufua Umeme (IPTL), Herbinder Seth, aameachiwa huru baada ya kutakiwa kulipa fedha TSh.Bil 26.9 kama fidia kwa Serikali huki akipewa masharti ya kutotakiwa kutenda kosa lolote kwa kipindi cha mwaka.

 

Hatua hi iyo imekuja  baada ya Seth kuingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) ya kumaliza kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inamkabili kwa njia muafaka.

 

Pia Seth amekubali kuweka hati ya kiwanda cha kufua umeme cha IPTL chenye namba 45566 kiwanja namba 292/2 kilichopo Kunduchi salasala kama dhamana iwapo atashindwa kulipa fedha hizo.

 

Hata hivyo, mshtakiwa Seth ameshalipa kiasi cha sh. Milioni 200 na kiasi kilichobakia anatatakiwa kukilipa ndanj ya miezi kumi na mbili kuanzia leo Juni 16, 2021.

Mshtakiwa Seth amesomewa upya mashtaka yake ambapo sasa ameshtakiwa na kosa moja la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kuondolewa mashtaka mengine 11 ambayo yalikuwa yakimkabili yeye na mshtakiwa mwenzake James Rugemalira ambaye ni Mkurugenzi mwenza wa IPTL amabye yeye bado anasota rumande.

 

Katika shtaka hilo jipya inadaiwa katika tarehe tofauti tofauti kati ya Novemba 29,2013 na Januari 2014 huko katika benki ya Stanbic Tawi la Kinondoni na benki ya biashara ya Mkombozi Tawi la St. Joseph ndani ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam mshtakiwa alitenda kosa.

Imedaiwa siku hiyo kwa njia ya udanganyifu mshtakiwa alijipatia kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) USD 22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post