Mwaka 1996, Jambazi Sugu Mtukutu Cheung Tze-Keung maarufu ‘Big Spender’ (Mtumia Pesa ) kutoka HongKong alimteka Victor Li Tzar-Kuoi ambaye ni Mtoto wa kiume wa Tajiri mkubwa nchini China Li Ka- Shing na baadaye akamuachia baada ya kupewa USD Milioni 130.
Baada ya kupewa pesa baadaye Jambazi huyo alimpigia simu Bilionea Li Ka na kumuomba ushauri wa jinsi gani afanye uwezekaji mzuri utakaofanya pesa hizo ziweze kumpa faida.
“Nilisikitika sana kwamba kamteka Mwanangu nimempa pesa na bado anapata ujasiri wa kunipigia ili nimpe ushauri wa jinsi ya kutumia fedha zangu, nilichomjibu ni kwamba nimempa pesa nyingi anazoweza kutumia hadi anaingia kaburini, kikubwa abadilike aache uhalifu na awe Mtu mwema, asipofanya hivyo kitu kibaya kitamtokea maishani”———-ni simulizi ya Bilionea Li wakati akihojiwa na Nanfang Media Group kutoka Guangzhou
Post a Comment