Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya leo Juni 28, 2021, inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi inayomkabili kada wa CHADEMA, Mdude Nyangali. Mdude anakabiliwa na mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin, gramu 23.4.
Juni 14, 2021, Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya iliahirisha kutoa hukumu dhidi ya kesi yake kwa kile kilichoelezwa kuwa hukumu bado haijakamilika pamoja na mambo mengine ambayo yalikuwa nje ya uwezo wa Hakimu.
Mdude anakabiliwa na makosa ya usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya Heroin kinyume cha sheria cha udhibiti dawa za kulevya namba 5 ya Mwaka 2015.
Post a Comment