Hamisa Mobeto Ala Shavu Serikalini.....Ubalozi wa Kodi




MWANAMITINDO na msanii Hamisa Hassan, maarufu kama hamisa Mobeto ateuliwa kuwa mmoja wa balozi wa kuhamasisha watu juu ya swala zima la ulipaji wa kodi leo 22 Juni 2021 bungeni jijini dodoma, waliochaguliwa engine ni Edo Kumwembe, Sammata

Waziri wa fedha na mipango Dkt.Lameck Mwigulu Nchemba leo bungeni jijini dodoma amemteua Mwanamitindo Hamisa mobeto kuwa mmoja wa mabalozi wa kuhamasisha watu kuhusu swala zima la ulipaji wa kodi.

Kupitia ukurasa instagram Hamisa mobeto ameposti na kuandika kwa kutoa shukurani kwa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na waziri wa fedha na mipango kwa kumuamini na kumteua kuwa balozi wa uhamasishaji wa ulipaji wa kodi.

Pamoja na kuwa na ubalozi wa kampuni tofauti tofauti kutangaza pedi kupitia HQ pads kutangaza urembo wa nywele za rasta kupitia kampuni ya Prima Afro siku ya leo bungeni Dodoma amepata shavu kubwa kwa kuteuliwa kuwa balozi wa kuhamasisha watu kwenye suala la zima la ulipaji wa kodi.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post