Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amemuapisha msanii Nickson Simon maarufu kama Nikki wa Pili kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe ambapo amechukua nafasi ya Jokate Mwegelo ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.
Baada ya kuapishwa kuwa mkuu wa wilaya kuna baadhi ya maswali yamekuwa yakiulizwa kuhusu hatma yake ya ushiriki kwenye Kampuni ya Weusi ambapo G Nako amefafanua hilo kwa kueleza kuwa.
"Taarifa ya kuteuliwa kwa Nikki niliifahamu baada ya mkeka kutoka, sikuwa na taarifa kabla teuzi sasa hivi itakuwa mapema sana kuzungumza kama kutakuwa na mabadiliko baada ya Nikki kupata majukumu ya Kiserikali lakini mabadiliko yatakuwepo kwenye muziki wa Weusi"
Tukio hilo la kuapishwa kwa Nikki wa Pili limefanyika leo Juni 21, 2021 kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani iliyopo Kibaha na alisindikizwa na mama wa mtoto wake Joan Temu 'Mama Zuri' na wasanii wenziye wanaounda Kampuni ya Weusi Joh Makini, G Nako Warawara na Lord Eyes.
Post a Comment