Fiston "Nipo Fiti Kuwamaliza Simba"




MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Abdoul Razack, amesema kuwa amejianda vema kuelekea mchezo wao dhidi ya Simba na yupo fiti kuwamaliza.


Kauli ya Fiston inakuja kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao utazikutanisha timu hizo Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.


Watano hao wa jadi, katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Novemba 7, 2020, walitoka sare ya bao 1-1.


Akizungumza na Spoti Xtra, Fiston amesema kuwa; “Upande wangu nipo salama, sina shida yoyote, nazidi kumuomba Mungu niwe salama siku hiyo ya mechi ili kuisaidia timu yangu.


“Nina imani timu yangu itaweza kushinda mchezo huo maana tumejianda vizuri na tunajiamini.“Najua ni mchezo wangu wa kwanza wa dabi hapa Tanzania, ila sina presha na mchezo huo maana nimecheza mechi nyingi sana kubwa na nikafanikiwa kuisaidia timu yangu, ingawa nafahu mechi itakuwa ngumu.”




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post