Cristiano Ronaldo na Lionel Messi kucheza pamoja





 RAIS wa Barcelona, Joan Laporta ana ndoto ya kuwakutanisha nyota wa Juventus, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi msimu ujao wa 2021/22 Barcelona na yupo tayari kutoa ofa ya wachezaji wawili katika juhudi za kuwashawishi mabosi wa mchezaji huyo raia wa Ureno.
 Licha ya kwamba mpaka sasa taarifa rasmi haijatolewa lakini Laporta anadaiwa kuwa na mpango wa kuwatoa wachezaji wawili ndani ya Barcelona kwenda Juventus.

Wachezaji ambao wanatajwa kuwa kwenye hesabu ya kutolewa ni pamoja na Griezmann, Sergi Roberto na Coutinho.

Nyota hao wote wawili, Messi na Ronaldo ni wachezaji wakubwa ambao wamekuwa wakishindana katika mafanikio ndani na nje ya uwanja. Msimu uliopita ndani ya La Liga, Messi alitupia jumla ya mabao 30 na mshikaji wake Ronaldo ndani ya Serie A alitupia mabao 29.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post