Klabu ya Soka ya Coastal Union (Wagosi wa Kaya), kutoka Jijini Tanga,mwenendo wao katika ligi Kuu ya Tanzania Bara (VPL),si mzuri na sio jambo la kushangaza iwapo watatokea wameshuka daraja msimu huu.
Hatua hiyo imekuja baada ya Timu hiyo kulazimishwa sare ya magoli 2-2, dhidi ya Timu ya soka ya Tanzania Prisons,katika dimba la Nelson Mandela, huko Sumbawanga Mkoani Rukwa June 22,2021 mchezo ambao ulichezwa majira ya saa kumi jioni.
Magoli ya Coastal Union yalifungwa na Abdul (23′) kwa mkwaju wa Penati na Mudathir (85′),huku yale ya Prisons yakifungwa na Samson (19′) Juma (36′),huku sare hiyo ikiwaacha Wagosi hao wa Kaya katika Nafasi ya 16 katika msimamo wa ligi Kuu Tanzania Bara,wakiwa na alama 34 baada ya kucheza michezo 31 na wamebakiza michezo 3 kabla ya kuhitimisha msimu huu.
By-BAKARI WAZIRI
Post a Comment