Chama Akubali yaishe, Aanza Upya



Kiungo mshambuliaji wa Simba Clatous Chama, amerejea kikosini kutoka nchini kwao Zambia baada ya kumaliza mazishi ya mke wake aliyefariki mwanzoni mwa mwezi huu.

Baada ya kurejea Chama amejiunga moja kwa moja kambini ambapo leo asubuhi amefanya mazoezi na wenzake kujiandaa na mchezo wa kesho wa ligi dhidi ya Mbeya City.

Wakati Chama akirejea kikosini kesho Simba itakosa  huduma ya mlinda mlango wake Aishi Manula na kiungo Taddeo Lwanga ambao wanatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Kocha msaidizi, Seleman Matola amesema baada ya kikosi kurejea jana kutoka jijini Mwanza kilipocheza mechi dhidi ya Polisi Tanzania kiliingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mechi ya kesho.

Matola amesema mchezo utakuwa mgumu kwa kuwa Mbeya City hawapo kwenye nafasi nzuri katika msimamo lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda ili kuzidi kusogelea ubingwa wa ligi kuu

“Kikosi kiliingia kambini jana baada ya kurejea kutoka Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu wa kesho na tunafurahi kiungo Clatous Chama amewasili na amejiunga na wenzake

“Manula na Taddeo wao watakosekana kwenye mchezo wa kesho sababu wana kadi tatu za njano wakati Ibrahim Ajibu ni mgonjwa anasumbuliwa na malaria lakini wachezaji wengine wote wako fiti tayari kwa mechi,” amesema Matola



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post