Watu watano wamefariki kwenye ajali iliyotokea usiku wakuamkia leo Juni 22, 2021 eneo la nanenane mkoani Morogoro na kuhusisha magari matatu ambayo ni Basi dogo aina ya Toyota Coaster, Lori na gari dogo aina ya Toyota Cresta.
Kamanda wa Polisi Morogoro Fortunatus Muslim amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa Coaster kutaka kuyapita magari yaliyopo mbele yake bila kuchukua tahadhari akitokea Dar es salaam kuelekea Mbeya kuzika akiwa amebeba mwili wa Marehemu pamoja na Abiria.
Kamanda Musilimu amesema hadi sasa bado haijafahamika idadi ya majeruhi lakini miili ya wote waliofariki ambao ni Wanaume watatu na Wanawake wawili imepelekwa Hospitalini.
Post a Comment