HitMaker wa wimbo wa 'Njiwa peleka salamu' Bi Patricia Hillary amefunguka kwamba wimbo huo aliurekodi mwaka 1980 lakini uzuri wa wimbo huo ukichezwa mahali ni kama umetoka siku za hivi karibuni.
Akizungumzia historia ya wimbo huo kwenye Heshima ya Planet Bongo ya East Africa Radio Hillary Patricia amesema
"Wasanii wa sasa waangalie tungo zao wanazotunga ziwe za muda mrefu, kama mimi njiwa peleka salamu nimeirekodi mwaka 1980 lakini mpaka sasa bado ina utamu wake"
"Nilimtumia njiwa kwa sababu ni ndege nzuri lakini wakati nauandika wimbo huo nilikuwa nimemshika mkononi na naongea nae kabisa, nilikuwa najisikia vizuri sana na watu walipenda huenda ndio alileta uzuri wa wimbo huo". ameeleza Bi Patricia Hillary
Post a Comment