Bahati Amfariji Mondi




MSANII wa nyimbo za injili kutoka Kenya, Kevin Bahati ‘Bahati’ amemfariji msanii mwenzie wa Bongofleva, Diamond Platnumz baada ya kushika nafasi ya tatu kwenye tuzo la BET kipengele cha ‘Best International Act’.

 

Bahati amemsifia Mondi kwa mafanikio mengi ambayo ameyapata katika tasnia ya burudani na kumtaja kama shujaa anayewapa vijana wa jamii ya Waswahili motisha wa kujitum katika maisha.

 

Kupitia akaunti ya mtandao wake Instagram, Bahati ameandika  “Kakangu  mkubwa Diamond Platinumz wewe bado ni mshindi. Umepata mafanikio mengi ukiwa na umri mdogo… mtu asikudanganye. Umewapatia watoto wengi wa jamii la Waswahili msukumo wa maisha na umewafanya kujua kuwa wanaweza kutoka nunge na kuwa shujaa.

 

“Umeshinda tuzo la BET tayari kupitia mkono wako mwingine; Rayvanny,Kaka turudi tena kazini na tutazamie makubwa zaidi, Grammys labda. Najivunia uwakilishaji wako wa jamii ya Waswahili. Simba asipo mshika swala hapungukiwi kuwa simba na kuwa fisi. Nakukumbusha kuwa wewe bado ni samba.”

 

Diamond aliibuka wa tatu kwenye tuzo ya BET ambayo ilinyakuliwa na nguli kutoka Nigeria, Burna Boy. Aya Nakamura wa Ufaransa, alikuwa wa pili kisha Diamond.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post