Amuua Mumewe, Amkata Nyeti na Kuzikaanga Kama Nyama





Kuna visa ukivisikia, lazima ujiulize mambo mengi sana. Dayane Machado (33); mdada wa nchini Brazil anaripotiwa kumuua mumewe kisha kumkata nyeti na kukaanga.

Chanzo cha yote imeelezwa Dayane alifanya hivyo baada ya kusalitiwa kimapenzi na mumewe, Andre kwa kwenda kuchepuka na mwanamke mwingine.

Wawili hao wana watoto wawili, wa kiume mwenye umri wa miaka nane na wa kike mwenye miaka mitano. Dayane na Andre wamekuwa pamoja katika penzi kwa miaka kumi, miaka miwili iliyopita waliachana, lakini wakawa wanarudiana na kuachana tena isivyo rasmi.

Siku ya tukio imeelezwa kuwa, wawili hao walikuwa kwenye ugomvi ambapo Dayane alitaka kuachana moja kwa moja na mwanaume huyo baada ya kuchepuka, lakini mwanaume hakukubali kuachwa na akawa anamtishia Dayane kuwa kama hataki kuwa naye, basi hataruhusu pia akawe na mwanaume mwingine zaidi yake.

Wakati wa mkwaruzano wao katika kujilinda imeelezwa Dayane alikwapua kisu na kuwahi kumuua mwanaume wake kisha kwa hasira, akaukata uume wake na kuukaanga.

Dada wa mume anasema anaamini wifi yake huyo alifanya mauaji hayo kulipiza kisasi baada ya mume kwenda kuchepuka. Dayane ametiwa mbaroni na vyombo vya sheria.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post