Amuua Mkewe kwa Kumtupia Nyoka Cobra





MWANAMKE mmoja ambaye alilipa mahari kubwa ili aolewe, lakini matokeo yake akaambulia kifo kwa mwanaume aliyemuoa

Kuna jamaa kwa jina anaitwa Sooraj (27) ambaye alijikuta akitiwa mbaroni na Jeshi la Polisi nchini India kwa kusuka mpango na kumuua mkewe, Uthra (25) ili arithi mali za mke.

 

Jamaa huyo alidaiwa kumuua mkewe huyo kwa kumrushia nyoka aina ya cobra aliyemnunua maalum kwa mpango huo.

Awali, Februari, mwaka huu, mume huyo alinunua nyoka aina ya viper mwenye sumu kali pia ili kumuua mkewe, lakini nyoka huyo alimng’ata Uthra ambaye alilazwa hospitalini karibia miezi miwili akitibiwa.

 

Mke huyo alipotoka, alirudi kwanza kwa wazazi wake ili afya yake itengamaye, lakini mume huyo naye alijifanya kwenda kuwa karibu na mkewe kumbe lengo lake ni kumuua kwa nyoka mwingine aina ya cobra wa Kihindi ambaye alimfungulia chumbani mkewe akiwa usingizini huku yeye akitazama nyoka huyo hadi alipomng’ata mkewe mara mbili ambapo alipokimbizwa hospifalini, madaktari walisema tayari amefariki dunia na kuacha mtoto wao mmoja mwenye mwaka mmoja.

 

Mwanamke huyo alikuwa anatoka familia inayojiweza na ndiye alitoa mahari ili aolewe na jamaa huyo, alitoa mahari ya sarafu za dhahabu karibia 100, gari jipya na Dola za Kimarekani 20,000 ambazo ni zaidi ya milioni 46.2 za Kitanzania.

 

Baada ya mkewe tu kufariki dunia, jamaa huyo akaanza kujimilikisha mali za mkewe, wazazi wa mke waliingiwa na shaka kwa tukio la mwanzo la mtoto wao kunusurika kufa kwa nyoka na sasa kufa kwa kuumwa na nyoka mwingine ndipo wakatoa taarifa Polisi.

 

Uchunguzi wa Polisi ulibaini kuwa jamaa huyo alimuua mkewe ili arithi mali kwa sababu kumpa talaka mke ilimaanisha arudishe pia mahari kubwa aliyopewa kumuoa. Jamaa huyo alitaka pia kuoa mwanamke mwingine aliyempenda aitwaye Sooraj anayefanya kazi benki binafsi ingawa familia yake haina uwezo na yeye binafsi kipesa hakuwa sawa ndiyo akataka kurithi mali za mkewe.

 

Rafiki yake aliyemuuzia nyoka hao wa mauaji na yeye pia alitiwa mbaroni na Polisi, uchunguzi wa Polisi pia ulibaini ndani ya miezi mitatu ya mpango huo, Sooraj alikuwa akitazama video za nyoka kwenye Mtandao wa YouTube kupitia simu yake ili kujua namna ya kubeba nyoka.

Stori Sifael Paul


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post