Mahakama nchini Marekani imemhukumu, Derek Chauvin aliyekuwa afisa wa polisi, kifungo cha miaka 22 jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua Mmarekani mwenye asili ya Afrika, George Floyd.
Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa Chauvin alimuua Floyd May 22, 2020 katika eneo la Minneapolis nchini humo kwa kumkandamiza na goti shingoni.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji alisema, “hukumu hii unayopewa inatokana na uhalisia kuwa ulitumia vibaya nafasi yako na imani uliyopewa. Pia, ulionesha ukatili katika kitendo ulichofanya.”
Floyd aliyekuwa na umri wa miaka 48, aliuawa na afisa huyo wa polisi baada ya kumuwekea goti kwenye shingo akiwa chini kwa zaidi ya dakika tisa.
Katika hukumu hiyo pia, Chauvin amezuiwa kutumia tena silaha ya moto na amesajiliwa katika orodha ya wahalifu wakatili.
Mahakama hiyo pia imewahukumu wenzake watatu kwa kosa la kukiuka haki ya msingi ya kiraia dhidi ya George Floyd.
Mauaji ya Floyd yalizua sintofahamu kubwa nchini Marekani ambapo wanaharakati walihamasisha wananchi kupitia kampeni ya ‘I can’t breathe’ kupinga vitendo hivyo.
‘I can’t breathe’, ikiwa na maana ya ‘siwezi kupumua’, ni neno alilokuwa analitumia George Floyd wakati askari huyo alipokuwa amekandamiza shingo yake kwa goti hadi alipopoteza maisha.
Post a Comment