Teknolojia ya uuzaji wa muziki kwa njia ya kidijitali ni sehemu ya uuzaji ambayo imezidi kuwa kubwa kwa miaka ya hivi karibuni hapa nchini kutokana na watumiaji wa huduma hiyo kuendelea kuongezeka kila siku.
Picha ya msanii Harmonize
Wasanii hutumia majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii kwa ajili ya kukuza kipato, bidhaa na huduma zao ambapo imekuwa rahisi kwa walaji ambao ni watumiaji wa vifaa vyenye uwezo wa kupata internet kama simu, kompyuta kupata product muda wowote.
Hawa ni baadhi ya wasanii wa kitanzania wenye Extended Pla (EP) na album ambazo zimefanikiwa kupata wasikilizaji wengi zaidi kupitia mtandao wa audiomack ambalo ni jukwaa la ku-stream muziki bila kikomo;
1.Harmonize – Afro East (Milioni 12.5).
2.Diamond Platnumz – A Boy From Tandale (Milioni 10.9)
3.Rayvanny – Sound From Africa (Milioni 10.3)
4.Jux – The Love Album (Milioni 10.2)
5. Zuchu – I Am Zuchu (Milioni 8.76)
6.Mbosso – Definition Of Love (Milioni 7.66)
7.Darassa – Slave Becomes A King (Milioni 3.85)
8. Ibraah – Steps EP (Milioni 2.14)
9. Navy Kenzo – Story Of The African Mob (Milioni 1.98)
10.Weusi – Air Weusi (Laki 603)
Post a Comment