Pesa na maajabu yake. Pesa ina maajabu yake hasa pale mtu akiipata. Wapo baadhi ya watu wakipata pesa kila mtu atajua tu, kwamba leo mzee Kira anapesa.
Baada ya kuona utangulizi mfupi basi karibu sasa uzifahamu tabia za wanaume wenye pesa kama ifutavyo;
Kuna wanaume wana pesa, wanajua kuzisaka, lakini pesa zao hazifanyiwi jambo la maana. Anaweza amka na million 1 asubuhi, lakini jioni akarudi hana hata mia mbovu. Pesa yote imeishia kwenye starehe. Wanapenda show off, wanapenda bata, wala hawawazagi kesho.
Kuna wanaume wenye kipato kidogo, lakini ni wavivu wa kujituma, akipata hela kidogo basi hafanyi kazi mpaka iishe. Wao kila jambo wanategemea msaada kwa ndugu, wala hawazi kuhusu maendeleo.
Kuna wanaume smart, wanajua nini wanakitaka kwenye maisha. Wanajituma, wanawekeza, na kamwe hawachoki kutafuta. Pesa zao zinafanyiwa mambo ya maana, wana ndoto, wana maono, wanahustle kuzitimiza.
Mwanamke mwenye akili timamu, kabla ya kuingia kwenye ndoa, lazima atahakikisha anapata mwanaume namba 3.
Awe na kipato kidogo au kikubwa, hakikisha mwanaume unayemchagua awe mume wako wa ndoa basi awe na sifa zifuatazo "Sio mvivu, ana ndoto, anajituma, anaishi kwa malengo, haendekezi starehe.
Na mwanamke asiyejitambua, lazima atamtaka mwanaume namba 1 kwavile tu anadanganyika na pesa anazopewa kipindi cha uchumba, kutolewa out, kupelekwa club mbalimbali, kununuliwa pombe, nakadhalika.
Na mwanamke anaye endeshwa kihisia huwa anachagua mwanaume namba 2 kwavile kampenda kwa dhati.
Huku moyoni mwake akiwa na imani kuwa wanaweza kujituma na wakakuza uchumi wao pamoja.
Nani kasema uchumi unakuzwa na wavivu
Post a Comment